Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili MDAs na LGAs – Desemba 2025
TAARIFA RASMI – OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia waombaji kazi wote walioomba nafasi mbalimbali za kazi kupitia mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kuwa wameitwa kwenye usaili kuanzia tarehe 15 Desemba 2025 hadi 22 Desemba 2025.
Tangazo hili linawahusu waombaji wa kada mbalimbali chini ya MDAs & LGAs, kama ilivyoainishwa kwenye Ratiba ya Usaili hapa chini.
1. Taarifa Kuu
Mtoaji wa Tangazo:
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs
Kumb. Na.: JA.9/259/01/C/10
Tarehe ya Tangazo: 03/12/2025
Muda wa Usaili: Kuanzia 15/12/2025 hadi 22/12/2025
Eneo la Usaili:
- Mikoa yote ya Tanzania Bara
- Vituo mahsusi Zanzibar (Unguja na Pemba)
Maelezo Muhimu:
Majina ya walioitwa kwenye usaili pamoja na vituo vyao vitapatikana kupitia tovuti:
➡ www.ajira.go.tz, kulingana na Mkoa anapoishi msailiwa (Current Resident Region).
2. Ratiba ya Usaili kwa Kada
| Mwajiri | Kada | Tarehe | Muda |
|---|---|---|---|
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III B – Fizikia | 15/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III C – Kilimo | 16/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Msaidizi wa Hesabu Daraja la II | 16/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Afisa Sheria Daraja la II | 17/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mhandisi Kilimo Daraja la II | 17/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Msanifu Majengo Daraja la II | 17/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III B – Hisabati | 17/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II | 18/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III B – Kilimo | 18/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daraja la II | 18/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Fundi Sanifu Daraja la II – Kilimo | 18/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mhasibu Daraja la II (Accountant Grade II) | 18/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III B – TEHAMA | 18/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III C – Hisabati | 19/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Afisa Mifugo Daraja la II | 19/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la IIIC – Fizikia | 19/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III C – TEHAMA | 19/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III B – Baiolojia | 22/12/2025 | 07:00 |
| MDAs & LGAs | Mwalimu Daraja la III C – Track Event | 22/12/2025 | 07:00 |
3. Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
A. Vya Kuleta
- Barakoa (Mask).
- Kitambulisho halali (chochote kati ya hivi):
- Kitambulisho cha Mkazi
- Kadi ya Mpiga Kura
- Kitambulisho cha Kazi
- Kitambulisho cha Uraia
- Pasipoti
- Leseni ya Udereva
- Barua ya Serikali ya Mtaa/Kijiji
Vyeti Halisi vinavyohitajika:
- Cheti cha Kuzaliwa
- Vyeti vya Kidato cha IV & VI
- Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada, n.k.
- Kada zinazohitaji usajili wa bodi: Leta vyeti halisi vya usajili na leseni za kazi.
B. Mambo Yasiyoruhusiwa
Wasailiwa hawataruhusiwa kuendelea na usaili wakileta:
- Testimonials
- Provisional Results
- Statement of Results
- Results Slips za Form IV & VI
C. Gharama na Mazingira ya Usaili
- Kila msailiwa atajigharamia usafiri, chakula na malazi.
- Vaa mavazi nadhifu na yenye staha, kama Waraka wa Mavazi unavyoelekeza.
D. Wasailiwa Waliosoma Nje ya Nchi
- Vyeti lazima viwe verified na:
- TCU
- NACTVET
- NECTA
- Kwa kada zinazohitaji GPA: Leta cheti cha ukokotozi kutoka TCU.
E. Tofauti ya Majina
- Leta Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
F. Kuthibitisha Taarifa
- Ingia kwenye Ajira Portal kukopi namba ya usaili.
- Kwa usaili wa mchujo wa mtandaoni: hakikisha unakumbuka email na password yako.
- Kama jina lako halipo kwenye orodha, angalia kwenye akaunti yako sababu.
4. PDF Downloads
- TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MDAs NA LGAs – 03/12/2025
PDF
5. Tahadhari kwa Watafuta Ajira
Sekretarieti ya Ajira haijihusishi na malipo ya aina yoyote.
⚠ Usitoe fedha kwa mtu yeyote kwa ahadi ya kupangiwa kazi, kupangiwa kituo, au kufanyiwa usaili.


3 responses to “KUITWA KWENYE USAILI MDAs NA LGAs”
Habari zamida na itwa jefta ni dereva
LikeLike
hello nafasi zote za kazi zinawekwa huku na namna ya kutuma maombi unaelekezwa pia
Asante
LikeLike
LikeLike