KUITWA KWENYE USAILI MDAs NA LGAs

Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili MDAs na LGAs – Desemba 2025

TAARIFA RASMI – OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia waombaji kazi wote walioomba nafasi mbalimbali za kazi kupitia mfumo wa Ajira (Recruitment Portal) kuwa wameitwa kwenye usaili kuanzia tarehe 15 Desemba 2025 hadi 22 Desemba 2025.

Tangazo hili linawahusu waombaji wa kada mbalimbali chini ya MDAs & LGAs, kama ilivyoainishwa kwenye Ratiba ya Usaili hapa chini.


1. Taarifa Kuu

Mtoaji wa Tangazo:
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs

Kumb. Na.: JA.9/259/01/C/10

Tarehe ya Tangazo: 03/12/2025

Muda wa Usaili: Kuanzia 15/12/2025 hadi 22/12/2025

Eneo la Usaili:

  • Mikoa yote ya Tanzania Bara
  • Vituo mahsusi Zanzibar (Unguja na Pemba)

Maelezo Muhimu:
Majina ya walioitwa kwenye usaili pamoja na vituo vyao vitapatikana kupitia tovuti:
www.ajira.go.tz, kulingana na Mkoa anapoishi msailiwa (Current Resident Region).


2. Ratiba ya Usaili kwa Kada

MwajiriKadaTareheMuda
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la III B – Fizikia15/12/202507:00
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la III C – Kilimo16/12/202507:00
MDAs & LGAsMsaidizi wa Hesabu Daraja la II16/12/202507:00
MDAs & LGAsAfisa Sheria Daraja la II17/12/202507:00
MDAs & LGAsMhandisi Kilimo Daraja la II17/12/202507:00
MDAs & LGAsMsanifu Majengo Daraja la II17/12/202507:00
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la III B – Hisabati17/12/202507:00
MDAs & LGAsAfisa Ufugaji Nyuki Daraja la II18/12/202507:00
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la III B – Kilimo18/12/202507:00
MDAs & LGAsAfisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daraja la II18/12/202507:00
MDAs & LGAsFundi Sanifu Daraja la II – Kilimo18/12/202507:00
MDAs & LGAsMhasibu Daraja la II (Accountant Grade II)18/12/202507:00
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la III B – TEHAMA18/12/202507:00
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la III C – Hisabati19/12/202507:00
MDAs & LGAsAfisa Mifugo Daraja la II19/12/202507:00
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la IIIC – Fizikia19/12/202507:00
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la III C – TEHAMA19/12/202507:00
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la III B – Baiolojia22/12/202507:00
MDAs & LGAsMwalimu Daraja la III C – Track Event22/12/202507:00

3. Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

A. Vya Kuleta

  • Barakoa (Mask).
  • Kitambulisho halali (chochote kati ya hivi):
    • Kitambulisho cha Mkazi
    • Kadi ya Mpiga Kura
    • Kitambulisho cha Kazi
    • Kitambulisho cha Uraia
    • Pasipoti
    • Leseni ya Udereva
    • Barua ya Serikali ya Mtaa/Kijiji

Vyeti Halisi vinavyohitajika:

  • Cheti cha Kuzaliwa
  • Vyeti vya Kidato cha IV & VI
  • Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada, n.k.
  • Kada zinazohitaji usajili wa bodi: Leta vyeti halisi vya usajili na leseni za kazi.

B. Mambo Yasiyoruhusiwa

Wasailiwa hawataruhusiwa kuendelea na usaili wakileta:

  • Testimonials
  • Provisional Results
  • Statement of Results
  • Results Slips za Form IV & VI

C. Gharama na Mazingira ya Usaili

  • Kila msailiwa atajigharamia usafiri, chakula na malazi.
  • Vaa mavazi nadhifu na yenye staha, kama Waraka wa Mavazi unavyoelekeza.

D. Wasailiwa Waliosoma Nje ya Nchi

  • Vyeti lazima viwe verified na:
    • TCU
    • NACTVET
    • NECTA
  • Kwa kada zinazohitaji GPA: Leta cheti cha ukokotozi kutoka TCU.

E. Tofauti ya Majina

  • Leta Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

F. Kuthibitisha Taarifa

  • Ingia kwenye Ajira Portal kukopi namba ya usaili.
  • Kwa usaili wa mchujo wa mtandaoni: hakikisha unakumbuka email na password yako.
  • Kama jina lako halipo kwenye orodha, angalia kwenye akaunti yako sababu.

4. PDF Downloads

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MDAs NA LGAs – 03/12/2025
    PDF

5. Tahadhari kwa Watafuta Ajira

Sekretarieti ya Ajira haijihusishi na malipo ya aina yoyote.
Usitoe fedha kwa mtu yeyote kwa ahadi ya kupangiwa kazi, kupangiwa kituo, au kufanyiwa usaili.

3 responses to “KUITWA KWENYE USAILI MDAs NA LGAs”

Leave a reply to Salumu Mwalimu Cancel reply