NAFASI 5476 ZA MAFUNZO VETA

Nafasi 5,476 za Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA – Desemba 2025
Tarehe: 5 Desemba 2025
Chanzo: Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi


Utangulizi

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano inatekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi, mpango maalum unaolenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata ujuzi wa stadi za kazi ili washindane ipasavyo katika soko la ajira. Kwa mwaka huu, serikali imetangaza nafasi 5,476 za mafunzo ya ufundi stadi, yatakayotolewa kupitia vyuo 46 vya VETA vilivyoidhinishwa nchini.

Mafunzo haya yanagharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali kwa upande wa ada. Mwanafunzi / Mzazi / Mlezi atahitajika kugharamia tu nauli na gharama ndogo binafsi.

Pakua Tangazo (PDF) hapa
PAKUA PDF HAPA


Fani Zinazotolewa

Mafunzo yanatolewa katika fani mbalimbali zikiwemo:

  • Urembo na Ususi
  • Ushawaji wa nguo & Ubunifu wa mitindo
  • Ufundi bomba
  • Uashi
  • Fundi magari
  • Ujenzi
  • Useremala
  • Uungaji vyuma
  • Uchomeleaji
  • Upakaji rangi
  • Maandishi ya alama
  • Upishi
  • Utengenezaji wa vipuri vya mitambo
  • Umeme wa majumbani na viwandani
  • Umeme wa magari
  • Umeme wa jua (solar)
  • Huduma za hoteli na utalii
  • Ukataji madini
  • Ufundi vyuma na fani nyingine zinazohusiana

Mafunzo haya yatafanyika hadi tarehe 26 Januari 2026.


Vituo Vilivyopitishwa

Vyuo 46 vya VETA vimeidhinishwa rasmi kutoa mafunzo haya katika fani husika. Orodha ya vyuo inapatikana kupitia tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu:

www.kazi.go.tz


Masharti ya Kujiunga

Mwombaji anatakiwa kuwa:

  • Mtanzania
  • Na umri kati ya 15 – 35
  • Mwenye afya njema
  • Mwenye elimu ya msingi au zaidi kwa fani nyingi za ufundi (urembo, ushonaji, uchomeleaji, useremala, uashi, n.k.)
  • Kwa fani zinazohitaji elimu ya sekondari, mwombaji awe amemaliza Kidato cha Nne au zaidi
  • Vijana wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na watapewa kipaumbele

Jinsi ya Kuomba

Maombi yanapokelewa kuanzia:

📅 05 – 19 Desemba 2025

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye Chuo cha VETA kilichopo mkoani wanakoishi:

  1. Barua ya maombi ya mafunzo
  2. Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
  3. Nakala ya Cheti cha Elimu (elimu ya msingi au sekondari kulingana na fani)
  4. Kitambulisho cha uraia / kadi ya mpiga kura (kwa wenye miaka 18+)
  5. Barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji
  6. Picha 4 za passport zilizoandikwa majina nyuma

Uteuzi wa Waombaji

Waombaji wote watakaokidhi vigezo vyote vilivyotajwa ndiyo watakaopangiwa nafasi katika mafunzo haya.


Hitimisho

Hii ni fursa muhimu kwa vijana kupata ujuzi wa ufundi stadi unaotakiwa kwenye soko la ajira. Kwa kuwa mafunzo yamegharamiwa kikamilifu na Serikali, vijana wanahimizwa kuchangamkia nafasi hizi mapema kabla ya muda kuisha.

One response to “NAFASI 5476 ZA MAFUNZO VETA”

Leave a comment